N'na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini ndiyo diwani iliyompatia Mohammed Khelef Ghassani tuzo ya Fasihi ya Kiafrika kwa Kiswahili inayotolewa na Mabati-Cornell mwaka 2015. Ni mkusanyiko wa tungo za mshairi huyu juu ya maisha ya ugenini, hisia za mhamiaji na maana ya kuishi kwenye dunia mbili kwa wakati mmoja.